NINA HAJA NAWE (I Need Thee Every Hour)
Nina haja nawe, kila saa;
Hawezi mwingine, kunifaa.
Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
Nina haja nawe; Kaa nami,
Na maonjo haya, Hayaumi.
Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
Nina haja nawe; Kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.
Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
Nina haja nawe; nifundishe,
Na ahadi zako, zifikishe.
Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
Nina haja nawe; Mweza yote;
Ni wako kabisa, Siku zote.
Yesu, nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
No comments:
Post a Comment